ZINAZOVUMA:

FIFA yaiondolea adhabu kitayosce

Shirikisho la mpira duniani FIFA limeiondolea adhabu klabu ya mpira...

Share na:

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea klabu ya Kitayosce adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji.

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kumlipa madai yake yote Kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman.

Awali Kocha huyo raia wa Misri aliishitaki FIFA klabu hiyo kwa kumvunjia mkataba kinyume cha taratibu.

Kwa hatua hiyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeiondolea Kitayosce FC adhabu ya kufungiwa kusajili.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya