ZINAZOVUMA:

Onana kurejea tena kuitumikia timu yake ya Taifa ya Cameroon

Golikipa wa Manchester United Andre Onana amekubali kurejea tena kuichezea...

Share na:

Golikipa wa Manchester United, André Onana kupitia tovuti ya klabu yake ametangaza kusitisha maamuzi yake ya kustaafu soka la Kimataifa na sasa atajiunga na timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Burundi Septemba 12, 2023.

Onana alistaafu soka la Kimataifa baada ya kutofautiana na Kocha Mkuu wa Cameroon, Rigobert Song wakati wa Kombe la Dunia mwaka jana nchini Qatar.

Itakumbukwa, baada ya kucheza mechi ya ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Uswizi, Onana aliondolewa kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Serbia ambapo golikipa huyo aliondoka kambini kabla ya kutangaza kustaafu akiwa na miaka 26 pekee.

Katika taarifa yake, Onana aliandika kuwa “Katika ulimwengu wa soka, kama katika maisha, nyakati za maamuzi hutokea ambazo zinahitaji maamuzi muhimu kufanywa. Katika miezi ya hivi karibuni, nimekuwa nikikabiliwa na majaribu yanayodhihirishwa na ukosefu wa haki na udanganyifu. Hata hivyo, upendo wangu usiotikisika na ushikamanifu wangu kwa nchi yangu, Cameroon, bado upo”,

“Hamu yangu ya kuiwakilisha nchi yangu haijawahi kuyumba tangu ujana wangu, na matarajio haya yanabaki kuwa sehemu isiyoweza kutenganishwa ya utambulisho wangu.

“Ninajibu wito wa taifa langu kwa uhakika usiotikisika, nikifahamu kwamba kurudi kwangu sio tu, kuheshimu ndoto yangu lakini pia kujibu matarajio na uungwaji mkono wa Wacameroon”.

Hayo ni miongoni mwa aliyoandika mchezaji huyo raia wa Cameron.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya