ZINAZOVUMA:

NSSF kuuza mradi wa kigamboni kurudishwa fedha zilizowekezwa

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF unatarajia kuuza...

Share na:

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu ya Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni).

Mradi huo uliopo Kigamboni jijini Dar es salaam unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kwa uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Septemba 25, 2023 jijini hapa.

Mshomba amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

“Kwa sasa mfuko kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali unakamlisha taratibu za zabuni baada ya kukamilika kwa hatua ya tathmini ya zabuni na maafikiano ya bei. Matarajio ni kusainiwa kwa mkataba wa mauzo ya mradi huu kabla ya tarehe 31 Oktoba 2023,” amesema Mshomba.

Bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana lakini alieleza kuwa wanaamini kuwa mnunuzi ataendelea kama ilivyokuwa imekusaudiwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya