N’Golo Kante, kiungo mahiri anayejulikana kwa uwezo wake wa kipekee na sifa zake za kibinadamu, amechukua usukani wa Royal Excelsior Virton, klabu iliyoko nchini ubelgiji karibu na mpaka wa Luxembourg.
Uhamisho rasmi wa umiliki kutoka kwa Flavio Becca kwenda kwa N’golo Kante unawakilisha tukio muhimu kwa klabu hiyo na umepokelewa kwa shauku kubwa kutoka kwa jamii ya wanasoka.
Pamoja na kuwa Kante anajiandaa kujiunga na klabu ya Al-Ittihad ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia baada ya kufanya vizuri na klabu kubwa ya Chelsea, bado haikumfanya nyota huyo wa mpira wa miguu kuingia mazima kununua klabu hiyo ya Ubelgiji.
Kwa sasa Royal Excelsior Virton inafuatilia kupata leseni yake ya itakayoiwezesha kushiriki katika Ligi daraja la pili ya Ubelgiji katika msimu wa 2023-24. Ligi hiyo ipo chini ya ligi ya Ubelgiji kwa daraja mbili.
Ni vyema kufahamu kwamba klabu hiyo imedai kuwa haina madeni, na ununuzi wa Kante utaongeza msukumo mpya katika jitihada zao za baadaye.
Safari ya Kante kuelekea umaarufu ilianza katika ngazi za chini za soka nchini Ufaransa, ambapo vipaji vyake vilivutia Caen, ambao walimsaini mwaka 2013.
Baadaye, alicheza alipambana katika ushindi wa Leicester City katika Ligi Kuu ya England msimu wa 2015-16 kabla ya kuhamia Chelsea, Stamford Bridge.
Alipofika Chelsea pia hakulaza damu Kante walitwaa ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya , Ligi Kuu, Ligi ya Europa, na Kombe la FA.
Zaidi ya hayo, mchango wa Kante ulienea nje ya soka ya klabu, kwani alikuwa sehemu muhimu ya ushindi wa Kombe la Dunia na timu ya taifa ya Ufaransa mwaka 2018.
Mafanikio yake ya kuvutia uwanjani na nje ya uwanja yamemfanya awe mtu anayeheshimika sana katika ulimwengu wa soka.
Hivi sasa kumekuwa na wimbi la wacheza mpira wa kulipwa kununua klabu. Hivi karibuni, Wilfried Zaha alishtua dunia kwa kushirikiana na mwanamuziki Stormzy waliponunua AFC Croydon Athletic.
Matukio kama haya yanaonyesha dhamira yao kwa mchezo huo na kwamba bado wana kitu wanategemea kukifanikisha.
N’Golo Kante kununua Royal Excelsior Virton ni nukta muhimu kwa klabu hiyo ya Ubelgiji.
Wakati Kante anajiandaa kwa sura mpya katika kazi yake na Al-Ittihad, ameazimia kushiriki kama mwenyekiti wa Excelsior Virton ili kukuza mafanikio ya klabu hiyo.