ZINAZOVUMA:

NETANYAHU: Israel itaendelea na operesheni licha ya kukatazwa

Netanyahu ang'ang'ania operesheni yake ya kibabe juu ya mashambulizi ya...

Share na:

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Jumapili kwamba wanajeshi wa Israel wataendelea na mashambulizi ya ardhini yaliyopangwa katika mji wa kusini wa Rafah. Mashambulizi hayo yamezua hofu katika ukanda wa Gaza huku wengi wakihofia kusababisha mauaji makubwa ya raia.

“Hakuna shinikizo la kimataifa litakalotuzuia kufikia malengo yote ya vita, kuondoa Hamas, kuwaachilia mateka wetu wote na kuhakikisha kuwa Gaza haitakuwa tishio tena kwa Israeli,” Netanyahu aliambia mkutano wa baraza la mawaziri katika video iliyotolewa na afisi yake.

“Ili kutimiza hayo, tutafanya pia operesheni huko Rafah,” alisema.

Maoni yake yamekuja huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza tena mjini Doha, Qatar, kutafuta makubaliano ya amani huko Gaza, ambapo Israel imeendeleza mashambulizi ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi mitano.

Wajumbe wa baraza la mawaziri la Israel walipanga kujadili “mamlaka” ya timu ya mazungumzo baadaye Jumapili, afisi ya Netanyahu imesema. Netanyahu alitarajiwa kukutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye alitarajiwa kusisitiza onyo lake dhidi ya mashambulizi ya ardhini ya Rafah.


Watu milioni 2.4 wa Gaza wametafuta hifadhi kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel katika mji huo wa kusini. Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye ameiunga mkono Israel wakati wa vita, amesema uvamizi wa Rafah “haukubaliki” isipokuwa pawe na mipango madhubuti ya kulinda raia.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya