ZINAZOVUMA:

Necta Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Sita 2023: Ufaulu wa Jumla Waongezeka

Baraza la mitihani Tanzania Necta limetangaza matokeo ya kidato cha...

Share na:

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) imetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 huku yakionyesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo jana Alhamisi Julai 13, 2023 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa ni 47, 340 na wavulana 59, 543.

Jumla ya watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2023 wamefaulu,” amesema.

Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.

Mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Ili kuona matokeo hayo, tembelea ukurasa hapo chini au bofya kiungo hiki: Bofya hapa

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya