ZINAZOVUMA:

Nape awataka wahariri kutoa elimu matumizi ya mitandao.

Waziri Nape Nauye amezungumza na wahariri wakati akifungua mkutano wa...

Share na:

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari, Mhe Nape Nnauye (MB) amewapongeza wahariri wa Tanzania kwa kufanya mkutano wa kitaaluma wa wahariri kwa miaka 12 mfulululizo ili kuhakikisha wanaboresha sekta ya habari hapa nchini.

Mhe Nape ameyasema hayo leo Machi 29, 2023 kwenye mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri utanaofanyika kwa siku tatu (3) Mkoani Morogoro, ambapo ameeleza kwa kiasi kubwa kesi za ufungiwaji wa vyombo vya habari umepungua. Pia amewataka wahariri kutoelimu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ili kutoa taarifa zenye tija kwa wananchi.

Aidha Mwenyekiti wa Wahariri Tanzania ndugu Deudatus Balile ameeleza hali ya uchumi kwa baadhi ya vyombo vya habari si nzuri hususani kwa magazeti yaliyofunguliwa mwaka 2021. Pia ndugu Balile amesema anaipongeza wizara kwa kazi kubwa inayoifanya kushirikiana na waandishi wa habari kuhakikisha wandishi wanapata uhuru wa vyombo hivyo. Mkutano huo umeshirikisha waandishi wa habari na wahariri kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali Tanzania.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,