ZINAZOVUMA:

Nafaka ndio njia ya Vilipuzi Ukraine – Urusi

Urusi yagundua kuwa vilipuzi huingia Ukraine kwa meli za kubeba...
Bandari ya Odessa

Share na:

Ofisi ya Usalama nchini Urusi (FSB) imekuta kuna viashiri vya vilipuzi katika meli ya kubebea shehena ya nafaka.

Meli hiyo inayotokea Uturuki ikielekea Rostov kwa ajili ya ajili ya kubeba nafaka, ilikaguliwa na kuzuiwa isiendelee na safari yake.

Huku taarifa hiyo iksema kuwa sababu ya kuzuia meli hiyo ni viashiria vya vilipuzi vilivyoonekana katika ukaguzi.

Shirika hilo la usalama nchini humo limesema “meli hiyo iliktia nanga nchini Ukraine katika bandari ya Kiliia mwezi Mei, huenda ilitumika kupeleka vilipuzi nchini Ukraine.

Katika taarifa yao wamesema kuwa meli hiyo ilibadili jina la meli, na hata wafanyakazi wa ndani katika bandari ya Tuzla nchini Uturuki.

Sababu ya kuzuiwa meli hiyo ni wasiwasi wa kuwa inawezekana ikawa imetumika kuleta vilipuzi ndani ya Ukraine.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya