ZINAZOVUMA:

Mwenza wa kamala atembelea J.K park.

Mwenza wa Makamu wa Raisi wa marekani Kamala Harris, Douglas...

Share na:

Bwana Douglas Emhoff mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris leo Machi 30, 2023 ametembelea Kituo Cha kukuza Vipaji vya Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park, kilichopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki pamoja na Mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani Bw. Emhoff na kupata fursa ya kufanya ziara fupi kuona jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na vijana wanaofundishwa mpira wa Miguu na Kikapu katika Kituo hicho.

Bw. Emhoff amewasihi vijana hao wajifunze kwa ari na bidii ili waje kuwa nyota wazuri na wakubwa Duniani.

Kwa upande wake Mhe. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Mwenza huyo kwa ziara yake katika Kituo hicho ambapo amesema ni miongoni mwa vituo vinavyolea vipaji ambavyo vinatarajiwa kuisaidia nchi katika Sekta ya michezo.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango kwa wadau ndani na nje ya nchi kuona fursa zilizopo nchini katika Sekta za Michezo, Utamaduni na Sanaa na kuzitumia katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,