Mwandishi wa vitabu kutoka Ghana Ama Ata Aidoo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Mwandishi huyo ambaye mbali na kuwahi kushikilia nafasi ya uwaziri wa elimu katika nchi yake ya Ghana mwaka 1982, pia alikuwa akifundisha fani ya uandishi bunifu kwenye vyuo mbalimbali duniani.
Mwandishi huyo ameandika vitabu vingi vya hadithi na vimekuwa vikitumika katika shule mbalimbali kama visaidizi katika masomo ya fasihi ukanda wa magharibi mwa Afrika.
Afrika ina waandishi wengi sana, Marehemu Ama Ata Aidoo ni miongoni mwao ila ni wachache wanaozijua na waliowahi kusoma kazi zao za uandishi.
Je umewahi kusoma kazi gani ya uandishi kutoka afrika iliyoandikwa na mama huyu?