ZINAZOVUMA:

MWANAHARAKATI WA KIMAREKANI AFARIKI

Daniel Ellsberg, mchambuzi wa ya masula kijeshi wa Marekani aliyevujisha...

Share na:

Daniel Ellsberg, mchambuzi wa ya masula kijeshi wa Marekani aliyevujisha siri nyingi za Vita vya Vietnam zilizojulikana kama “Pentagon Papers”, amefariki akiwa na miaka 92 huko nyumbani Kensington, California siku ya ijumaa.

Taarifa hizo za siri alizofichua zilionyesha udanganyifu mkubwa wa serikali ya marekani uliosababisha kupiganwa vita vya Vietnam na kusababisha maafa makubwa duniani.

Ellsberg, aligunduliwa kuwa na saratani ya kongosho isiyoweza kupona kwa upasuaji mwezi Februari kulingana na taarifa kutoka katika familia yake.

Ellsberg aliwafahamisha wamarekani juu ya udanganyifu unaweza kufanywa na serikali yao na pia amekuwa mstari wa mbele na kuwatetea wale wote wanaopingana na harakati hizo za uzushi wa serikali hiyo.

Uvujaji wa siri hizo za “Pentagon papers” ulionyeshwa katika filamu maarufu ya “The Post” ya mwaka 2017.

Dunia imeona watu wengi kama ellsberg waliokuja baadae kama Edward Snowden na julius Assange wa Wikileaks.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya