ZINAZOVUMA:

Mvua kubwa zaendelea kuitesa India

Zaidi ya watu 24 wamepoteza maisha kufuatia mvua kubwa zinazoendelea...

Share na:

Mamlaka nchini India, imesema takriban watu 24 wamepoteza maisha huku tisa kati yao wakifariki baada ya hekalu kuporomoka na wengine wakiwa hawajulikani waliko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.

Mvua hiyo imekua ikisababisha mafuriko, kusombwa kwa magari, kubomoa majengo na kuharibu madaraja katika majimbo ya kaskazini ya Uttarakhand na Himachal Pradesh.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi ni ya kawaida na husababisha uharibifu mkubwa wakati wa msimu wa mvua kubwa nchini India, lakini wataalam wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza kasi kwa hivi sasa yanafanya hali kuwa mbaya zaidi.

Sukhvinder Singh Sukhu, Waziri Mkuu wa jimbo lililoathiriwa zaidi Himachal Pradesh, amesema watu wasiopungua 16 wamepoteza maisha katika muda wa saa 24 zilizopita, wakiwemo tisa katika tukio la kuanguka kwa hekalu la Kihindu katika mji mkuu wa jimbo la Shimla.

Aidha Sukhu alitoa wito kwa wakazi wa Jimbo hilo kukaa ndani na kuepuka kwenda karibu na mito wakati huo Shule zote zikitakiwa kufungwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya