Linhas Aéreas de Moçambique (LAM), Shirika la ndege la Msumbiji limeakhirisha safari za ndege 5 kutokana na uhaba wa mafuta.
Shirika hilo la ndege limeakhirisha safari hizo siku ya jumapili ya tarehe 11 mwezi February 2014, ambapo maelfu ya wasafiri wameathirika na mzozo huo.
Huku makampuni ya mafuta yakidaiwa kukataa kuwapa mafuta kutokana na deni kubwa wanalodaiwa.
Baadhi ya wasafiri ambao walipoulizwa walisema kuwa shirika hilo halikuwapa taarifa ya kuahirishwa kwa safari zao.
Safari zilizoahirishwa ni Maputo kwenda Harare na Lusaka ambazo ni za kimataifa, na nyingine ni Maputo kwenda Pemba, Quelimane na Inhambane ambazo ni za ndani ya Msumbiji.
Deni la mafuta la shirika hilo limefikia Meticai milioni 600 sawa na Dola za marekani Milioni 9.5) kwa kampuni ya Umma Petromoc, na deni lao kwa PUMA ni Meticai milioni 42.
Viwango vya kubadili fedha US$1 = Meticai 63.5