ZINAZOVUMA:

Mnangagwa ampa uwaziri mwanae

Mtoto pamoja na mpwa wa Emerson Mnangagwa, Raisi wa Zimbabwe,...
Mtoto wa Mnangagwa akiapa

Share na:

Raisi Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe, hivi karibuni amepata ridhaa ya wananchi wake kuongoza kwa muhula wa pili katika nafasi hiyo.

Katika kuteua mawaziri na manaiu waziri, Raisi Mnangagwa amemteua mwanae David Kudakwashe Mnangagwa kuwa Naibu Waziri.

Mnangagwa mdogo mwenye umri wa miaka 34, atashikilia wadhifa wa Naibu Waziri wa Fedha nchini humo.

Pia katika baraza hilo, Raisi mnangagwa amemteua mpwa wake Tongai Mnangagwa, kama Naibu waziri wa Utalii.

Kitendo hicho cha raisi huyo kuteua nduguze katika nyadhifa hizo, kimepigiwa kelele na upinzani kama ambavyo ushindi wake katika uchaguzi mkuu umekuwa ukipigiwa kelele.

Kuhusu wateule hao wa Raisi mnangagwa, naibu waziri wake wa fedha, David Kudakwashe Mnangagwa alisoma Shahada ya Sheria katika chuo kikuu cha Zimbabwe, na kusoma Shahada ya usimamizi wa biashara (“Actuarial Science”) Drake University.

Yupo katika bodi mbalimbali ikiwemo benki ya National Building Society (nbs), ni mjasiriamali, pia ni muwekezaji.

Kuhusu naibu waziri wa Utalii alisoma Astashahada ya Masoko katika chuo cha Harare Polytechnic, na kwa sasa anasoma Shahada ya Maendeleo katika Chuo Kikuu Huria cha Zimbabwe.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya