ZINAZOVUMA:

Mmomonyoko wa maadili umefanya vijana wasiaminike

Makamu wa Rais amesema maadili kwa vijana nchini yameporomoka jambo...

Share na:

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amesema maadili kwa baadhi ya vijana nchini yameporomoka jambo linalowafanya washindwe kuaminika.

“Ni neno lenye ukakasi kulisema lakini ngoja niseme tu, kwamba vijana wengi wa nchi yetu maadili yao yameporomoka, wengi hawana uzalendo na Taifa lao, hawana uadilifu, wavivu na wamejawa na tamaa ya kupata fedha kwa haraka,” alisema Dkt Mpango.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kongamano la siku mbili la vijana wa Mkoa wa Dodoma ambalo lilikusanya washiriki 3,500 kutoka wilaya zote saba za mkoa linalofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini hapo.

Lengo la kongamano hilo ni kuwafanya vijana watambue fursa zinazowazunguka na kuzichangamkia ili kujiajiri na kuondokana na hali ya kulalamika kuhusu kukosa kazi.

Dkt Mpango alisema kukosa uaminifu kwa vijana kunawafanya washindwe kuijenga Tanzania ya sasa na kesho wakati wanategemewa pindi wazee watakapokuwa wamechoka.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,