ZINAZOVUMA:

Mkutano kujadili mabadiliko ya mifumo ya chakula Afrika

Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula barani Afrika umeanza rasmi...

Share na:

Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula ya Afrika (AGRF) 2023 unatarajiwa kuanza leo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ambapo utakutanisha maelfu ya washiriki wakiwemo viongozi wa serikali, wanasayansi, wawekezaji, watunga sera, wakulima na vijana kutoka mataifa zaidi ya 70.

Mkutano huo wa siku nne, utalenga zaidi kujadili mabadiliko ya mifumo ya chakula na kuhakikisha uhakika wa chakula kwa wote.

Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza na kujadili na viongozi wa mataifa mbalimbali, wataalamu, wawekezaji, vijana na wengineo juu ya namna Afrika inaweza kuendeleza na kuja na njia mbadala ili kunufaika na kilimo cha chakula.

Mambo yanayotarajiwa kuzungumzwa ni pamoja na kutafuta suluhu ya changamoto zinazokabili mataifa ya Afrika katika upatikanaji wa chakula ikiwemo athari za mabadiliko ya tabia nchi, Wataalamu watashauri na pia kuangalia njia bora ya kunufaika na miradi endelevu ya kilimo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,