ZINAZOVUMA:

Mjumbe wa UN aliyetumwa Sudan ajiuzulu

Mjumbe kutoka umoja wa mataifa aliyechaguliwa kwenda Sudan amejiuzulu huku...

Share na:

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes ambae ni raia wa Ujerumani ametangaza kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mjumbe huyo ametahadharisha juu ya hatari ya kuwepo kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe kutokana na migogoro inayoendelea Sudan.

“Namshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nafasi hii na kwa imani aliyoiweka kwangu, lakini nimemwomba anipunguzie kazi hii,” Perthes amesema.

Aidha ameweka wazi kuwa kilichoanza kama mzozo kati ya makundi mawili ya kijeshi kinaweza kugeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo kamili.

Na kusisitiza kwamba mapigano hayaonyeshi dalili za utulivu na hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kwa suluhu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya