ZINAZOVUMA:

Mgombea wa Urais apigwa risasi Ecuador

Mgombea wa nafasi ya urais nchini Ecuador amepigwa risasi tatu...

Share na:

Mgombea wa kiti cha urais nchini Ecuador, Fernando Villavicencio amepigwa risasi na kuuawa wakati wa hafla ya kampeni huko Quito siku ya Jumatano.

Maafisa wa polisi nchini humo wamesema tukio hilo ni uhalifu wa kupangwa uliotekelezwa na watu wenye nia ya kuondoa maisha ya mgombea huyo.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 59 alipigwa risasi kichwani mara tatu wakati akijiandaa kuondoka kwenye mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa Ecuador, mshauri wake wa kampeni, Carlos Figueroa aliviambia vyombo vya habari vya ndani, akithibitisha kifo cha bosi wake.

Rais Guillermo Lasso ambae ndio Rais wa sasa wa Ecuador amelaani kufanyika kwa tukio hilo katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Lasso amesema kuwa amechukizwa na kushtushwa na mauaji ya mgombea urais Fernando Villavicencio na kuongeza kuwa “uhalifu wa kupangwa umeenda mbali sana,” na akasema mauaji hayo yatafuatiliwa.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya