ZINAZOVUMA:

McDonalds Malaysia yafungua kesi

McDonalds Malaysia imefungua kesi hiyo baada ya kampeni za kususia...

Share na:

Tawi la Malaysia la mgawaha maarufu duniani wa McDonalds, umefungua kesi ya madai kwa asasi ya kraia ya BDS Malaysia.

Kesi hiyo imejikita katika madai ya kuwa kampeni za asasi hiyo dhidi ya vita vya Gaza vimechafua mgahawa na kuharibu biashara yake.

Mgahawa huo umedai fidia ya dola za marekani milioni 1.3, kwa kuharibiwa hadhi na soko kibiashara.

Mgahawa huo umejiweka mbali na uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza kwa kusema kuwa “Hawaungi mkono Israel , wala kuunga mkono mzozo huo wa Mashariki ya kati”.

Kampeni za BDS zimekuwa zikilenga kususia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Israel au zinazozalishwa na kampuni zinazomilikiwa na wazayuni au zile zenye kuunga mkono Israel katika uvamizi wa Gaza.

Katika majibu dhidi ya kesi hiyo kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X BDS ilichapisha “tunakataa kabisa hili” wakiashiria hawakuikshifu McDonalds.

Miongoni mwa kampuni zilizowekwa katika orodha ya kususiwa na BDS ni pamoja na Caltex (Mafuta na vilainishi vya mashine), HP (Vifaa vya elektroniki), Caterpillar (Mitambo mikubwa), Puma (Nishati).

Mbali na kampeni za BDS kususia bidhaa za kampuni mbalimbali, pia serikali ya Malaysia imezuia meli za Israel kuingia katika bandari zake iliyotolewa Disemba 21 2023.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya