ZINAZOVUMA:

Mbunge ataka tembo wachinjwe wapelekewe nyama

Munge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Ruvuma aitaka Wizara...

Share na:

Mbunge wa Viti Maalum Dk Thea Ntara, ameitaka serikali kuchinja tembo na wanayama wengine wakorofi wanaovamia makazi ya watu, na nyama hizo wapewe wananchi wanaokula nyama hiyo.

Katika mifano ya wananchi wa Tanzania wanaokula nyama ya tembo ametaja wakazi wa mkoa wa Ruvuma.

Wazo hilo alilitoa wakati akichangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2024/25, iliyosema kuwa kuna maeneo kuna wanyama wanaovamia makazi ya watu.

”Lakini pia Mheshimiwa Waziri, suala la tembo, Ruvuma tunakula sana nyama yake. Hebu niwaombe kama mnafikiria kupunguza, muwachinje sijui niseme kuwaua, halafu tengenezeni hizo nyama, pelekeni mikoa ambayo wanaliwa” alisema Dk. Ntara.

“…Mjipange kuhusu hawa wanyama wanaoua wapunguzeni, sisi tupo tayari kula hiyo nyama,” amesema Mbunge huyo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya