Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema huwezi ukaiandika historia ya Lowassa ukaliacha neno Chadema, huku akisema alitumikia chama hicho kwa miaka minne.
“Nimesikiliza na nimeisoma sana historia ya Lowassa kama ambavyo imewasilishwa, mimi binafsi ni mtu mkweli na nimesikitika kwa sababu amefanya mambo mengi makubwa ndani ya Serikali ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ndani ya vyama vya upinzani katika Taifa letu sote,”amesema Mbowe.
Mbowe amesema Lowassa alianza na safari ya matumaini katika Chama Cha Mapinduzi nakuhamia kwenye safari ya mabadiliko Chadema.
Kiongozi huyo amesema hayo leo Februari 17, 2024 kwenye maziko ya waziri mkuu huyo mstaafu aliyefariki Februari 10 mwaka huu.