ZINAZOVUMA:

Mbeya: Ahukumiwa miaka 30 kisa mapenzi ya jinsia moja.

Kijana mwenye umri wa miaka 22 amehukumiwa miaka 30 baada...

Share na:

Mahakama ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Claud Mwinuka (22) maarufu kama ‘Kibakuli’ baada ya kukiri kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Hukumu hiyo imesomwa jana Alhamisi Aprili 6, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Paul Barnabas baada ya mtuhumiwa kufikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Amesema Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kukiri kosa la kuruhusu kuingilia kinyume na maumbile na wanaume, huku akijua ni kosa la kifungu cha 154 kifungu kidogo cha kwanza (C) cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Hakimu Barnabas amesema wametoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanajihusisha na tabia hiyo.

Awali inadaiwa mtuhumiwa alisambaza picha za video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa amevalia mavazi ya kike huku akitembea usiku wa manane ambapo alikamatwa na sungusungu waliokuwa doria na kufikisha katika vyombo vya dola.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya