Nyota wa PSG Kylian Mbappe amekataa ofa ya Al-Hilal ya Saudi Arabia ya kujiunga nao kwa mkataba wa mwaka mmoja licha ya klabu yake kukubari na kuiruhusu Al-Hilal kufanya mazungumzo nae.
Al-Hilal iliweka ofa nzuri ambayo ingevunja rekodi ya dunia ya usajili wa mchezaji, hata hivyo imeonekana bado Kylian Mbappe ana malengo ya kucheza barani Ulaya kama ambavyo iliripotiwa hapo awali.
Hatua hiyo inazidi kuiweka katika wakati mgumu klabu ya PSG kwani kama hakutakuwa na klabu nyingne ya Ulaya itakayomtaka mchezaji huyo italazimika abakie hapo mpaka mwakani ambapo atauzwa bure.
Kylian Mbappe hana mapenzi tena na klabu yake ya PSG na aligoma kuongeza mkataba mwingine kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Ufaransa.
PSG misimu ya hivi karibuni ilifanya usajili mkubwa na kufanikiwa kuwa na nyota wa kubwa kama vile Neymar, Messi pamoja na Mbappe lakini licha ya kuwa na wachezaji wote hao pamoja hawakufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya.