ZINAZOVUMA:

Mashirika ya mazingira Kenya yaishtaki ‘Total Energies’

Mashirika ya mazingira nchini Kenya yameishtaki kampuni ya mafuta ya...

Share na:

Total Energies, Kampuni ya Mafuta ya nchini Ufaransa Imeshitakiwa na Mashirika manne ya ulinzi wa mazingira, yakidai inachangia athari za tabia nchi kutokana na mradi wake wa bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania.

Yakiongozwa na Darwin Climax Coalitions na Sea Shepherd France pamoja na mashirika mengine mawili, yanataka mradi huo kusitishwa.

Mawakili wa Mashirika hayo wakiongozwa na William Bourdon wamesema kesi hiyo imewasilishwa dhidi ya kampuni hiyo ya Total Energies ya nchini Ufaransa tangu Septemba 22.

Katika kesi hiyo mashirika hayo yanasema ujenzi wa mradi huo utasababisha uharibifu mazingira, mali na kuhatarisha maisha ya watu wa nchi hizo mbili.

Mbali na wanaharakati hao, Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linataka pia kusitishwa kwa ujenzi huo wenye urefu wa Kilomita 1,445 kutoka Hoima nchini Uganda hadi kwenye Bandari ya Tanga nchini Tanzania, wenye thamani ya Dola Bilioni 10.

Licha ya shinikizo hizi, Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameapa kuwa ni lazima mradi huo uendelee, huku kampuni ya Total Energies ikisema watu zaidi ya Laki Moja watakaothiriwa na mradi huo wamelipwa fidia.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya