ZINAZOVUMA:

Mashabiki 4 wa Namungo wapoteza maisha kwenye ajali

Basi lililokuwa limebeba mashabiki wa timu ya Namungo kutoka Ruangwa...

Share na:

Mashabiki wa timu ya Namungo inayoshiriki ligi kuu kutoka Ruangwa wamepata ajari ya gari wakiwa safarini kuelekea Dar es salaam kushuhudia mchezo baina ya timu yao na klabu ya Yanga unaofanyika jumatano ya tarehe 20 Septemba,2023.

Ajali hiyo imetokea eneo la Miteja karibu na Somanga na kupelekea vifo vya mashabiki wanne na majeruhi kumi na sita.

Majeruhi wote katika ajali hiyo Kwasasa wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi Wilaya ya Kilwa, Lindi ambako ndipo wanapopatiwa matibabu.

Aidha Klabu ya Namungo inatoa pole kwa wanaruangwa, mashabiki familia na kwa wote waliopata ajali hiyo na majeruhi ikiwaombea wapone haraka.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,