Nchi ya Japan ndio mwenyeji wa mkutano wa mataifa ya G7 ambao unafanyika kuanzia leo tarehe 19 mpaka tarehe 21, ambao unahudhuriwa na viongozi wa nchi za Canada, Italy, France, Germany, Uingereza pamoja na marekani.
Huu ni mkutano wa pili wa G7 kutawaliwa na uvamizi wa Ukraine, na huku usiku kucha wa kuamkia leo kampeni za uvamizi wa anga ya Urusi ziliendelea.
Hata hivyo mkutano huo wa G7 umezindua vikwazo vipya dhidi ya nchi ya Urusi ambavyo vimewasilishwa na Taifa la Marekani.
Aidha taarifa zinasema kuwa Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anatarajia kuhudhuria mkutano huo wa G7 ili kujadili uvamizi uliofanywa na Urusi nchini kwake.
Awali ilisemekana kuwa angejumuika nao kwa njia ya mtandao lakini taarifa mpya zinaeleza kuwa Raisi huyo atajumuika katika mkutano huo yeye mwenyewe na kuonana na viongozi wa G7 ana kwa ana.