ZINAZOVUMA:

Marekani yatishia kusitisha msaada wa kijeshi Misri

Misri inashutumiwa na watetezi wa haki za binadamu kuhusika na...

Share na:

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba mamlaka nchini Misri zimekua zikitumia mateso na yameenea sana mpaka kufikia kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika ripoti iliyowasilishwa kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso yanayofanyika, zaidi ya makundi sita yalizungumzia aina ya mateso wanayokutana nayo ikiwemo kupigwa, shoti za umeme, unyanyasaji wa kingono na kunyimwa huduma za matibabu.

Wengi ya waliokutana na mateso dhidi ya maafisa usalama wamesema mateso hayo yanatumika kama mbinu ya kisiasa kupunguza upinzani.

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti ya Marekani, Ben Cardin, ametishia kuzuia msaada wa kijeshi wa Marekani nchini Misri ikiwa haitachukua hatua madhubuti kuboresha rekodi yake kuhusu haki za binadamu.

Imeonekana ndani utawala wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi amekuwa akiwakandamiza zaidi wapinzani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya