ZINAZOVUMA:

Marekani yampongeza Raisi wa Senegali

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amempongeza...

Share na:

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amepongeza raisi wa Senegal Macky Sall kwa kutangaza uamuzi wa kutogombania muhula wa tatu katika uchaguzi wa raisi utakaofanyika mwakani.

Rais Sall alitangaza uamuzi wake wakati wa hotuba yake kwa taifa kupitia kituo cha televisheni ya taifa, na kuuzima uvumi wa miaka kadhaa, uliozusha ghasia na wasiwasi wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

“Senegal ni kubwa kuliko mimi, imejaa watu wenye uwezo wa kuipeleka katika hatua nyingine.”

Kwa upande wake Waziri Blinken alisema kwenye taarifa yake,

“Tunaamini kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki na mabadiliko ya mamlaka yataimarisha taasisi zenye nguvu na nchi yenye utulivu na ustawi zaidi. Tamko la wazi la Raisi Sall linaweka mfano katika kanda hiyo, tofauti na wale wanaotaka kuvuruga misingi ya kidemokrasia, pamoja na ukomo wa muda wa kuwepo madarakani.”

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,