ZINAZOVUMA:

Marekani na Afrika Kusini kuanza chanjo ya Ukimwi

Marekani na Afrika Kusini zitakua nchi za kwanza katika kufanya...

Share na:

Nchi za Marekani na Afrika Kusini zimetajwa kuwa zitaanza majaribio ya chanjo mpya ya kuzuia virusi vya Ukimwi (VVU) na tayari zimeanza kuwaandikisha washiriki watakaohusika kwenye majaribio hayo ambapo matokeo ya awali yatatangazwa mwaka 2024.

Shirika la NIH linalojihusisha na utafiti limesema kuwa chanjo hiyo inayoitwa VIR-1388 imetengenezwa mahususi kusaidia seli za mwili ambazo ni msaada mkubwa kwenye mfumo wa kinga kupambana na vijidudu na kuukinga dhidi ya magonjwa.

Vyombo vya Habari vimeripoti kuwa jaribio la chanjo hiyo linafadhiliwa na kampuni ya Marekani ya Vir Biotechnology, Taasisi ya Bill na Melinda Gates na Shirika la NIH ambalo linajihusisha na utafiti la Serikali ya Marekani.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya