ZINAZOVUMA:

Marekani imemuwekea vikwazo Jenerali Dagalo wa Sudan

Marekani imeamua kumuwekea vikwazo Jenerali wa RSF wa Sudan kwa...
Deputy head of Sudan's sovereign council General Mohamed Hamdan Dagalo speaks during a press conference at Rapid Support Forces head quarter in Khartoum, Sudan February 19, 2023. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Share na:

Marekani imemuwekea vikwazo kamanda wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan RSF Jenerali Hamdan Dagalo kutokana na vitendo vyake vya kusababisha machafuko na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanywa na wanajeshi wake katika mzozo baina yao na jeshi la Sudan.

Taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani imesema imemuwekea vikwazo kamanda huyo anayeongoza kikosi cha RSF kwa tuhuma za kuongoza kundi la wanajeshi wanaohusika na mauaji ya raia, mauaji ya kikabila na unyanyasaji wa kijinsia.

Kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa siku ya jana, chini ya vikwazo hivyo watazuia mali na vitu vyote vya Marekani vinavyomilikiwa na Dagalo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya