ZINAZOVUMA:

Mapya yajiri ugomvi kati ya Musk na Zuckerberg

Baada ya kushindikana kuingia ulingoni kupigana kati ya Elon Musk...

Share na:

Ugomvi unaoendelea kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Meta, Mark Zuckerberg na Mkurugenzi wa SpaceX, Elon Musk umechukua sura mpya baada ya Musk kumdhihaki Zuckerberg kwa kumwita ‘kuku’.

Hayo yanajiri baada ya Zuckerberg kutangaza kutofanyika pambano lao akiamini Musk hachukulii kwa ukubwa pambano hilo.

Awali akizungumzia pambano hilo Zuckerberg alisema: “Nadhani sote tunaweza kukubaliana kwamba Elon hayuko makini na ni wakati wa kuendelea na mambo mengine. Nilitoa tarehe halisi,” aliandika Zuckerberg kwenye Threads.

“Elon hajathibitisha tarehe, halafu anasema anataka kufanyiwa upasuaji, nakwenda kushindana na watu ambao wanachukulia michezo kwa ukubwa.” Aliongeza.

Ugomvi wa matajiri hao ulianza baada ya Mkurugenzi wa META Mark Zuckerberg kufungua mtandao wa kijamii wa Thread unaofanana sana na ule X au twitter ya zamani ulionunuliwa na Elon Musk.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,