ZINAZOVUMA:

Mameneja wa TEMESA kanda na Mikoa tumbo joto

Waziri Wa Ujenzi Innocent bashungwa kuwaweka tumbo joto mameneja wa...

Share na:

Waziri Innocent bashungwa wa Ujenzi, awaweka tumbo joto mameneja wa Kanda na Mikoa wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Hii ni baada ya kumtaka Mtendaji Mkuu wa TEMESA kuwasilisha orordha ya mameneja wa Kanda na Mikoa wasiofanya vizuri majukumu yao.

Bashungwa ametoa agizo hilo Aprili 22, 2024 jijini Dodoma, kufuatia kupokea malalamiko mara kwa mara juu ya huduma duni zinazotolewa na taasisi hiyo.

Katika malalamiko hayo pia kimeweka kivuko cha MV Tanga kilichopo mkoani Tanga, na kumuagiza Katibu Mkuu kufanyia kaziili kubaini changamoto zinazokwamisha kivuko hicho.

“Mambo mengi ya kiutendaji yanaletwa kwa Waziri na Katibu Mkuu wakati Watendaji mpo na tumewaamini kusimamia Taasisi zenu, hili jambo lipo sana kwenu”.

“Mtendaji Mkuu kama kuna mapungufu ya wasaidizi wako bora uje kwa Katibu Mkuu useme huyu hatufai, aondoke kuliko kukaa nao maana hatimaye litakuangukia wewe” Alisema Bashungwa.

Pia amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour kuangalia namna bora ya usimamizi wa TEMESA katika huduma ya vivuko nchini, ili kuleta manufaa na kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji.

Katika mambo aliyoyasisititiza ni kuwa taasisi hiyo bado ina mikwamo katika kutekeleza majukumu yake kwa uharaka pindi tatizo linapogundulika katika Vivuko, na hii ndio sababu ya kuzorota kwa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo.

“Changamoto ya marekebisho ya kivuko cha MV Tanga yanaendelea zaidi ya siku 10 sasa lakini leo naulizia vifaa bado havijafika, kama ‘parts’ ziko Dar es Salaam inachukua masaa mangapi hadi kufika Tanga? na sio Tanga pekee yake ni maeneo mengi yenye vivuko”, Aliuliza Waziri akimuhoji Mtendaji Mkuu wa TEMESA.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya