ZINAZOVUMA:

Mambo bado magumu Sudan.

Mazungumzo ya kutuliza ghasia nchini Sudan hayaonekani yakileta ahueni kwani...

Share na:

Mashambulizi ya anga yameutikisa tena mji mkuu wa Sudan Khartoum wakati mazungumzo ya kutafuta amani yakiendelea mjini Jeddah Saudi Arabia na kuonekana kutokuzaa matunda.

Mwanadiplomasia wa Saudia amesema pande zote mbili zinajiona zina uwezo wa kushinda vita suala ambalo linafanya mazungumzo hayo kuwa magumu na usitishaji vita wa kudumu kutokuwezekana.

Sudan ilitumbukia katika machafuko mabaya wakati mapigano yalipozuka tarehe 15 Aprili kati ya vikosi vya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al Burhan dhidi ya Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) ambapo mpaka hivi sasa zaidi ya watu 550 wamepoteza maisha yao na maelfu kujeruhiwa.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya