ZINAZOVUMA:

Mali yapiga marufuku shughuli za kisiasa na matangazo yake

Serikali ya Kijeshi nchini Mali imezuia vyombo vya habari kutangaza...

Share na:

Serikali ya kijeshi nchini Mali siku ya Alhamisi ilipiga marufuku vyombo vya habari nchini humo kutangaza miendendo ya kisiasa. Amri hiyo imekuja siku moja baada ya kuzuia shughuli za kisiasa nchini humo.

Sauti za upinzani zimezimwa kwa kiasi kikubwa tangu kanali Assimi Goita walipochukua mamlaka katika mapinduzi ya 2020, na kumpindua rais wa kiraia Ibrahim Boubacar Keita.

Mamlaka ya juu ya mawasiliano nchini Mali ilitoa taarifa Alhamisi kama wito kwa “vyombo vyote vya habari (redio, televisheni, vyombo vya habari vilivyoandikwa na mtandaoni) kusitisha utangazaji na uchapishaji wa shughuli za vyama vya siasa na shughuli za asili ya kisiasa ya vyama”.

Haikuonyesha kitakachotokea kwa mashirika ya vyombo vya habari ambayo hayakuzingatia marufuku hiyo.

Hatua hiyo imejiri baada ya mamlaka siku ya Jumatano kuamuru kusimamishwa kwa muda usiojulikana shughuli zote za kisiasanchini humo, na kusema kuwa serikali inahitajika kudumisha utulivu wa umma.

Msemaji wa serikali Kanali Abdoulaye Maiga alilaumu kusimamishwa kwa shughuli za kisiasa kutokana na “majadiliano tasa” wakati wa jaribio la mazungumzo ya kitaifa mapema mwaka huu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya