ZINAZOVUMA:

TCRA: Kumtag mtu picha chafu ni uhalifu

Katika mafunzo ya sheria ya uchaguzi kwa waandishi wa habari...

Share na:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka watumiaji wote wa mitandao ya kijamii, ambao wamekuwa wakikuta wameunganishwa (tagged) na picha chafu kwenda kutoka taarifa za matukio hayo Jeshi la Polisi.

Mamlaka hiyo imesema vitendo hivyo vimeshika kasi kwa sasa ni kosa kisheria na ni uhalifu kama uhalifu mwingine, ambapo wote waliojikuta wameunganishwa na picha hizo waende polisi kutoa taarifa, ili hatua kali zichukuliwe kwa wahusika.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Imelda Salu, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Simiyu, yaliyolenga kuwakumbusha sheria mbalimbali za habari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Mhandisi Imelda alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mtandao, ni kosa kisheria kumuunganisha mtu na Picha au taarifa chafu bila ya idhini yake na kitendo hicho kinahesabika kama uhalifu.

“ Tumeanza kuona vitendo vya mtu kumtag au kumuunganishamtu mwingne na picha chafu, watu wengi wanalalamika, kama mamlaka tunawaambia walioathirika na vitendo hivyo mamlaka ya kushughulika masuala hayo ni jeshi la polisi hivyo waende watoe taarifa,” amesema Mhandisi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya