ZINAZOVUMA:

Mali yahairisha uchaguzi kufanya mabadiliko ya katiba

Uongozi wa kijeshi nchini Mali umeghairi kufanya uchaguzi wa Urais...

Share na:

Serikali ya kijeshi ya Mali imeahirisha uchaguzi wa Rais ambao ulitarajiwa kurudisha taifa hilo la Afrika Magharibi kwenye demokrasia baada ya mapinduzi ya 2020.

Uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Febuari 2024, umeahirishwa ili kuruhusu serikali ya mpito kupitia taarifa za uchaguzi, kuruhusu vifungu vipya vya katiba ambavvyo vitachelewesha duru ya pili ya uchaguzi.

Ni mara ya pili kwa serekali ya kimapinduzi ya Mali ambayo imetokana na mapinduzi mwaka 2020 kuahirisha uchaguzi wa Rais wa nchi.

Wanasiasa wa Mali wamekosoa uamuzi huo ambao unaweza kusababisha vikwazo vya kiuchumi kwa Mali kutoka jumuiya ya mataifa ya Magharibi ECOWAS.

Jumuiya hiyo ililegeza vikwazo kwa Mali Julai 2022 baada ya serikali kuahidi kufanya uchaguzi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya