ZINAZOVUMA:

MALI YAFUKUZA VIKOSI VYA AMANI

Mamlaka ya kijeshi ya mpito nchini Mali siku ya Ijumaa...

Share na:

Mamlaka ya kijeshi ya mpito nchini Mali siku ya Ijumaa iliomba kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kwa kifupi “MINUSMA” kiondoke nchini humo “bila kuchelewa”, wakidai “mgogoro wa imani” kati ya mamlaka za Mali na kikosi hicho.

“Kwa bahati mbaya, MINUSMA inaonekana kuwa chanzo cha tatizo katika kuchochea mvutano katika jamii,” akinukuliwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop, aliiambia baraza lenye wanachama 15.

“Hali hii inasababisha kutokuaminiana miongoni mwa idadi ya watu wa Mali na pia kusababisha mgogoro wa imani kati ya mamlaka za Mali na MINUSMA,” alisema. “Serikali ya Mali inaomba kuondolewa kwa MINUSMA, bila kuchelewa.”

Hii inawakilisha hatua kubwa ya mabadiliko kwa nchi ya hiyo ya Afrika Magharibi, ambayo imekabiliana na uasi ulioenea huku wengine wakidai kujitenga tangu harakati hizo zilipoanza mwaka 2012. MINUSMA ilipelekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2013 kusaidia kurejesha utulivu nchini humo.

Kumekuwa na migongano baina ya Serikali hiyo ya kijeshi na kikosi hicho cha usalama pamoja na washirika wengine wa kimataifa kama Ufaransa kutokana na kutokuridhishwa kwa gali ya amani na utulivu nchini humo. Hali hii imechangiwa hasa na mapinduzi mawili yaliyotokea nchini humo mwaka 2020 na 2021 huku vikosi hivyo vikiwepo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya