ZINAZOVUMA:

TARI yavuka malengo uzalishaji mbegu.

Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania imevuka malengo ya tani...

Share na:

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kituo cha TARI- Hombolo kinaendelea na shughuli ya uzalishaji wa mbegu za Mtama ambapo kituo hicho kimezalisha zaidi ya tani 50 na kinaendelea na uzalishaji wa mbegu. Uzalishaji huo umevuka lengo la tani 40 ambayo kituo hicho ilijiwekea.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa kituo cha TARI- Hombolo Dkt. Joel Meliyo wakati akitoa tathmini juu ya hali ya Uzalishaji wa Mbegu za Mtama katika Mashamba ya kituo hicho Machi 28, 2023 Mkoani Dodoma.

Miongoni mwa aina ya Mbegu zilizozalishwa ni Macia yenye uwezo wa kustahimili hali ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa hazihitaji mvua nyingi na zina mavuno Mengi.

Kufuatia Hatua Hiyo Mkurugenzi Dkt. Meliyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imetoa fedha za kuzalishaji mbegu kupitia Mradi wa “Post Covid recovery”.⁩

Endelea Kusoma

Uchambuzi wa Maeneo ma 3 muhimu ya Kitajriba katika uteuzi huu wa

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya