ZINAZOVUMA:

Kila la heri Taifa Stars dhidi ya Moroco hivi leo

Hamna chembe ya shaka katika hili, kwani tumejionea tangu kuanza...

Share na:

Anaandikia Dkt. Ahmed Sovu

Katika kandanda au kabumbu au kipute cha Afrika(AFCON) Leo, tarehe 17/01/2024. Timu yetu ya Taifa itaanza rasmi mbio za kusaka ushindi dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco.

Timu yetu ya Taifa, inaingia katika mchezo huo ikiwa kwenye ari na mori wa aina yake katika michuano hiyo.

Hii imetokana na kuwapo kwa hamasa kubwa kutoka kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan viongozi mbalimbali, timu teule ya Hamasa na maombi ya Watanzania na hata ndugu zetu wengine katika Jumuiya ya Afrika ya Afrika Mashariki.

Ni matumaini yetu kuwa katika mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 2:00 usiku kwa saa za Tanzania, STARS wataibuka na ushindi dhidi ya taifa la Morocco. Ushindi ambao utawaweka sawa kisaikolojia dhidi ya mechi nyingine watakazozicheza baadae.

Hamna chembe ya shaka katika hili, kwani tumejionea tangu kuanza kwa mashindano haya makubwa ya Afrika, hata yale mataifa makubwa na maarufu kisoka yakianza kwa kusuasua.

Tumeshuhudia mahojiano yaliyofanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Damas Ndumbaro akisema kuwa kikosi cha wachezaji wa Stars kuwa wana ari, kani na wapo tayari kuwakabili na kupambana na timu za m Morocco, Zambia na DRC Congo katika kundi lao.

Tunatoa mwito kwa Watanzania wote kuongeza sala na dua dhidi ya STARS ili kuibuka na ushindi.

Kila la Heri, Taifa Stars Kila la heri vijana wetu. Viva Tanzania, Viva Stars. Apigwe Morocco apigwe.

igwe Morocco apigwe.

📍 AFCON ni yetu 🏆⚽▪️▪️

Endelea Kusoma

Uchambuzi wa Maeneo ma 3 muhimu ya Kitajriba katika uteuzi huu wa

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya