ZINAZOVUMA:

Majaliwa: Vifo vinavyotokana na maafa ya mvua vimevuka 150

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa vifo vilivyotokana na Mvua...

Share na:

Katika kipindi hii cha mvua kubwa zinazoendelea duniani kote, Tayari vifo zaidi ya 150 vimeripotiwa nchini Tanzania.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha kipindi cha mvua za masika nchini, zimeanza mwezi wa tatu na kunyesha kwa wingi huku ikiacha siku chache bila kunyesha.

Mbali na vifo hivyo pia mvua hiyo imesababisha maafa mbalimbali kama majeruhi zaidi ya 230, kuathiri zaidi ya watu laki 2 nchini kote pamoja na kuharibu nyumba takriban elfu 10.

Na taarifa hizi za maafa zimetokea katika mikoa 14 kati ya 26 ya Tanzania Bara.

Watu wengi katika mikoa hiyo wameathirika kwa namna moja ama nyingine, kwa kuharibiwa mazao, nyumba, kufa kwa wanyaa na hata kufariki kwa wapendwa wao.

Pia mvua hizo zimeharbu miundombinu mbalimbali nchini ikiwemo barabara, vituo vya afya, shule na madaraja.

Kutokana na maafa hayo tayari Serikali kupitia wakala mbalimbali imekuwa ikifanya ukarabati wa dharura au tathmini ya maafa ili kupanga bajeti ya ukarabati mkubwa nchini.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya