ZINAZOVUMA:

Mahujaji 1000 kulipiwa gharama zote za HIJJA

Mfalme wa Saudi Arabia na Msimamizi wa misikiti miwili mitakatifu...

Share na:

Msimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu duniani, Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud, ameagiza kuwalipia mahujaji 1,300 kutoka nchini zaidi 88 duniani kwa ajili ya Hijja mwaka huu.

Na mahujaji 1,000 katika hao wanatarajiwa kutoka katika familia za mashujaa, wafungwa na majeruhi wa kiPalestina.

Huku mahujaji 22 wakitoka katika familia za mapacha walioungana, ambao walitenganishwa nchini Saudi Arabia hivi karibuni.

Watu hawa 1300 watalipiwa gharama za hijja kwa mwaka huu 1445 sawa na 2024, kama sehemu ya mpango wa wageni wa Msimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu.

Mpango huo husimamiwa na kutekelezwa kila mwaka na Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo na Msimamizi wa mpango huo Sheikh Dr. Abdullatif bin Abdulaziz Al Al-Sheikh, alitoa shukran za dhati kwa Mfalme Salman na Muhammed bin Salman mrithi wa kiti cha Ufalme.

Al-Sheikh alibainisha kuwa tangu kutolewa kwa amri hiyo ya Kifalme, wizara yake imekuwa ikijiandaa kuwakaribisha mahujaji hawa na imeunda mpango mkakatina kamati kadhaa kuhudumia wageni hao.

Mpango huo unaanza mara tu mahujaji wanapoondoka katika nchi zao na kuhakikisha wanapata urahisi wote wa kutekeleza Umra na Hijja kwa wepesi, na kutembelea Madinah na kusali katika Msikiti wa Mtume.

Kulingana na waziri, tangu kuanzishwa kwake miaka 26 iliyopita, zaidi ya mahujaji 60,000 wamekaribishwa chini ya mpango huu.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya