ZINAZOVUMA:

Mahakama Nigeria imewaachia watuhumiwa LGBTQ

Mahakama nchini Nigeria imewaachia kwa dhamana watuhumiwa 69 wanaojihusisha na...

Share na:

Mahakama nchini Nigeria imewaachia kwa dhamana watuhumiwa 69 waliokamatwa mwezi uliopita kwa kujihusisha na ndoa za jinsia moja.

Kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa ya Afrika mahusiano ya jinsia moja yanaonekana ni utovu wa maadili, kinyume na tamaduni za Afrika na haikubaliki na dini.

Nigeria iliweka sheria dhidi ya watu wanaojihusisha na mahusiano ya jinsia moja toka mwaka 2014 licha ya katazo la kimataifa.

Aidha watu hao wameachiwa baada ya kulipa zaidi ya dola 645 kama dhamana mahakamani hapo.

Hata hivyo mwanasheria upande wa mashtaka alipinga kutolewa dhamana kwa watuhumiwa hao lakini haikufanikiwa sababu kosa hilo si miongoni mwa makosa ambayo hayana dhamana kwa sheria za Nigeria.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya