ZINAZOVUMA:

Magonjwa yasiyoambukiza yanaiathiri zaidi jamii

Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa...

Share na:

Zaidi ya shilingi bilioni 137 kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya zimetumika kugharamia magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha miaka mitano.

Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa mzigo mkubwa kwa jamii kutokana na fedha nyingi kutumika kugharamia
magonjwa hayo.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameyasema hayo katika kikao maalumu cha mafunzo kati ya wanahabari na wadau mbalimbali wa afya kinachofanyika leo Septemba 14 jijini Dar es Salaam.

Msigwa amewataka wanahabari kufikisha elimu kwa jamii kubadili mtindo wa maisha ikiwemo kuzingatia ulaji sahihi wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya