ZINAZOVUMA:

Apple Kuweka Mabadiliko ya Bei kwenye Programu ya “App Store” kwa Tanzania, Nigeria, Misri, na Uturuki

Nchi za Tanzania, Misri, Nigeria na Uturuki zimekumbwa na mabadiliko...
APP STORE
apple-app-store-logo

Share na:

Apple inatarajiwa kuleta mabadiliko ya bei katika programu yake ya “App Store” kuanzia tarehe 25 Julai 2023. Mabadiliko haya yatakuwa na athari kwa watengenezaji wa programu na watumiaji katika nchi tatu barani Afrika, Tanzania, Nigeria, na Misri, pamoja na nchi ya Uturuki barani Ulaya. Taarifa za mabadiliko haya zimetolewa na kampuni hiyo kupitia ukurasa wa tovuti yake.

Kulingana na taarifa hiyo, Tanzania itatozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya 18% na Kodi ya Mtandao ya 2%, huku Misri ikitozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani ya 14%. Uturuki nayo imeongezewa Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka 18% hadi 20%. Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja kodi ya ongezeko la thamani au kodi zingine kwa nchi ya Nigeria.

Mabadiliko haya yanatokana na mabadiliko ya hivi karibuni katika viwango vya kodi na viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa nchi hizo.

“Mfumo huu wa biashara mtandaoni na mfumo wa malipo wa App Store ulijengwa ili kukuruhusu kuanzisha na kuuza bidhaa na huduma zako kwa urahisi kwenye kiwango cha kimataifa, katika sarafu 44 na maduka mtandao 175. Wakati sheria za kodi au viwango vya ubadilishaji fedha vinabadilika, mara kwa mara tunahitajika kusasisha bei katika App Store kwa maeneo fulani na/au kurekebisha mapato yako,” ilieleza taarifa hiyo.

Mabadiliko haya yanalenga kuhakikisha uwiano sahihi wa bei za huduma zinazonunuliwa kupitia App Store kulingana na viwango vya ubadilishaji fedha vinavyokubalika.

Pata taarifa kamili kuhusu mabadiliko ya bei katika App Store na athari zake kwa Tanzania, Nigeria, Misri, na Uturuki.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,