Kampuni ya ‘M-Pesa holding company limited’ inayomiliki kampuni ya miamala ya fedha kwa simu M-pesa inatarajiwa kununuliwa kwa dola moja ya marekani ambayo ni sawa na shilingi 2405 za kitanzania.
Hata hivyo kampuni hiyo inayomilikiwa na shirika la simu la Vodafone la uingereza inanunuliwa na kampuni ya Safaricom ambayo pia inamilikiwa na shirika hilo hilo la Vodafone.
Sababu kuu ya kuuzwa kwa kampuni hiyo kwa Safaricom ni kurahisisha biashara na kuongeza ufanisi kama ilivyonukuliwa toka kwa mtendaji mkuu mpya wa shirika la Vodafone.
Mbali na sababu hiyo kumekuwa na maswali ikiwa matumizi ya fedha za M-Pesa yataendelea kusaidia jamii kama ilivyokuwa kwa Vodafone au yatabadilika katika umiliki wa Safaricom.