Shirikisho la mpira miguu Tanzania TFF Jana Agosti 30 limetangaza kikosi ambacho kimeiitwa timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria utakaochezwa Septemba 7, 2023.
Maoni mbalimbali juu ya kikosi hicho yametolewa na wadau wa michezo huku wengi wakijiuliza kwanini baadhi ya wachezaji hawajajumuishwa kwenye kikosi.
Miongoni mwa mchezaji anaetajwa sana kutojumuishwa kwenye kikosi ni Feisal Salum ambae ni mchezaji wa klabu ya Azam.
Wakati Feisal maarufu kama ‘Zanzibar finest’ alipokuwa na mgogoro na timu yake ya zamani ya Yanga na hakua akicheza kwa muda alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa lakini sasa ambapo anacheza uwanjani na inaonekana yupo kwenye kiwango bora hajajumuishwa kwenye kikosi.
Wadau mbalimbali wa michezo wametoa maoni yao wakikosoa uitwaji wa timu ya Taifa.
Kikosi cha TaifaStars kipo chini ya kocha mu Algeria Adel Amrouche ambae ndio anakiongoza katika michezo ya kufuzu AFCON.