ZINAZOVUMA:

Kope bandia zinapoteza uwezo wa kuona

Matumizi ya kope bandia na lenzi za miwani zinasababisha uoni...

Share na:

Wanawake wanaoweka kope bandia na wanaovaa lenzi za miwani bila kupima wako katika hatari ya kupata matatizo makubwa ya kuona kiasi cha kuhitaji upasuaji.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Dkt. Cyprian Tomoka amesema mtu yeyote anayetaka kuweka kifaa chochote mwilini mwake afanye vipimo kwanza ili kujua kama kitaendana na mwili wake ili kuepuka madhara.

Amesema watu wengi wamepata matatizo ya macho yaliyotokana na kuvaa miwani ambayo haijapimwa, kuweka kope na kuvaa lenzi machoni.

“Hata ukitaka kuweka lenzi ya kuonea au kope basi pima. afya ya macho yako kwa sababu tunapata wagonjwa ambao wanakuja kutibiwa macho yenye viashiria kwamba huyu aliweka kope bandia na huyu aliweka lenzi ya kuonea na mwingine anakuwa na vidonda machoni ingawa hawasemi,” amesema.

Aidha, amesema wagonjwa wengi wanachelewa kufika hospitalini mara wanapopatwa na matatizo hayo hali inayopelekea kupata vidonda machoni na hivyo kuwa katika hatari ya kupoteza uwezo wa kuona.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya