Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa bado wana ari ya kupambana na kupata matokeo yatakayowapeleka kwenye fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Usiku wa leo Manchester City watakuwa wenyeji wa Madrid kwenye nusu fainali mkondo wa pili baada ya sare ya bao moja nchini Hispania juma lililopita.
Kocha Ancelotti anasema lengo lake ni kupata mafanikio hivyo yupo tayari kwa changamoto yoyote na leo anatamani kuonesha hilo.
“kama ilivyo kawaida tutajaribu kupata kile kilicho bora kwa timu lakini pia kwa mtu binafsi, ninafikiri tunaweza kupata matokeo mazuri zaidi ya mkondo wa kwanza” alisema Ancellot.
Madrid ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo na wanalisaka taji lao la 15 la michuano hiyo