ZINAZOVUMA:

Klabu ya Simba yaja na ‘Back to school’

Klabu ya soka ya Simba imekuja na mkakati mpya WA...

Share na:

Klabu ya soka ya Simba imekuja na mkakati wa kutengeneza mashabiki wa baadae kwa kuamua kuwajumuisha wanafunzi wa shule katika michezo yao.

Programu hiyo imepewa jina la ‘Back to school’ ambapo lengo lake ni kuhakikisha wanatengeneza mashabiki ambao wataipenda Simba kuanzia wakiwa wadogo mpaka watakapokua.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula ambae amesema kuwa katika kila mechi ya Simba watawaalika watoto wa shule mbalimbali kuja kutazama na wataandaa maeneo maalumu kwa ajili yao.

Aidha ameeleza kwamba Simba itashirikiana na shule mbalimbali nchini ili kuwasaidia wanafunzi wanaopenda michezo katika kuboresha vipaji vyao.

Pia ameongeza kuwa ni muhimu kuwajali watoto katika michezo kwani inawafanya wawe timamu na pia kujenga nidhamu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya