Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Professor Kithure Kindiki ametuma onyo kali kwa upinzani kuelekea maandamano mengine yanayotarajiwa siku ya Jumatano.
Kithure amesisitiza kuwa hakuna aliye juu ya Sheria nchini Kenya na hatoruhusu uharibifukama uliofanyika Ijumaa iliyopita.
”Maafisa wetu wa usalama wapo tayari kumshughulikia yeyote aliye na nia ya kuharibu amani na mali za wananchi” amesema
Onyo hili limekuja baada ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kuandaa mkutano mfupi katikati ya Jiji ambapo amesema kwamba raia wamechoka na wapo tayari kwa lolote siku ya Jumatano.
Aidha Raila amemtaka Rais Ruto kuachia madaraka huku mchakato wa kukusanya saini milioni 10 kwa ajili ya kumng’atua madarakani ukitarajiwa kuanza kabla ya mwishoni mwa wiki hii.